Sunday, June 12, 2016

Google Wazindua App Mbili Mpya, "Allo" Na "Duo"


Tamasha kubwa linalo andaliwa na Google kila mwaka Google I/O lilifanyika jana likiwa linalenga mambo muhimu ambayo Google wanatarajia kuanzisha, mambo mapya yatakayo kuwepo kwenye android pamoja na vifaa vipya ambavyo google wanatarajia kuvianzisha.
Hili tamasha hurushwa live kupitia youtube ili hata mimi au wewe ambao tunaishi huku AFRICA tusipitwe na mambo mazuri ambayo Google wanatarajia kuyaleta kwenye maisha yetu.

Moja ya vitu ambavyo Google walizindua jana ni application mbili ambazo zitakuja kwenye android siku chache zijazo. Moja ya application ambayo iliwavutia watu wengi sana na kuwaacha midomo wazi ni Allo.

Allo ni chatting application kama ilivyo Whatsapp lakin hii ipo kipekee kabisa na itakuwa mpinzani mkubwa wa Whatsaap. Moja ya sifa kubwa ya hii app ni kupunguza muda wa ku type kwa kukupa smart reply. Mfano mtu akikikutumia picha ya mbwa, hii app ina uwezo wa kujua hiyo picha iliyotumwa ni kitu gani na inakupa reply za kuchagua kama nice dog, ugly dog etc.

Kitu kingine kizuri kuhusu Allo ni kuwa integrated (kuchanganywa) na Google Assistant. Hii ina maanisha kwamba ukiwa unatumia hii app na unataka ku search kitu kwenye google basi utaweza kufanya hapo hapo ukiwa ndani ya hiyo app. Hii ni tofauti kabisa na apps nyingine kama Whatsapp ambazo inakubidi utoke kwenye whatsapp uende kwenye google search halafu urudi tena kwenye whatsapp...mambo ya kizamani hayo...



Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top