Watumiaji Wengi wa simu za smartphone wamekuwa wakijiuliza tofauti ya 3g, H na H+
3G ndio Teknolojia mama ndani yake ndio unakuta teknolojia kama wcdma, hspa na hspa+
Simu ikionyesha 3G ujue hapo unatumia WCDMA
Simu ikionyesha H au 3.5G ujue hapo unatumia HSPA
Simu ikionyesha H+ au 3.75G ujue hapo ni HSPA+
tofauti zake hapo ni kwamba 3G inakaa na chaji na speed yake ni ndogo mara nyingi hutumika tu kama standby ukiwa hufanyi chochote inakaa hiyo.
H na H+ zenyewe zina speed kubwa, H+ ina speed zaidi lakini zinakula sana charge.
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini