Monday, July 4, 2016

Jinsi ya Kukoleza na Kulaza Herufi Kwenye Whatsapp


Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (Italic) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati (strikethrough) kwenye Whatsapp?

Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo jipya la app ya WhatsApp kwenye simu yako.

  • Jinsi ya Kuweka bold


Ili kukoleza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama hiyo hiyo ya nyota kwa mfano ukiandika *Renatus* itatokea ikiwa bold.


  • Jinsi ya Kuweka Italic


Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo (italic), unahitajika kutanguliza mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Kwa mfano ukiandika “_Renatus_” itatokea ikiwa Italics.



  • Jinsi ya Kuweka strikethrough (tide)


Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye maneno yako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi  [tilde (~)] na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Kwa mfano ukiandika “~Renatus~” itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.


  • Jinsi ya Kuunganisha mitindo


Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake  maandishi yako kuwa na bold, strikethrough na Italic kwa wakati mmoja utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno lako na kuhitimisha.
Mfano, ukiandika *_~Renatus~_* inafaa kutokea ikiwa bold-italics pamoja na strikethrough.


Share na wenzako wapate kujua ujanja huu..
Nakutakia siku njema





Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top