Monday, August 29, 2016

Whatsapp Kutuma Data Zako Kwenda Facebook


WhatsApp walikuwa wanapinga kwa muda mrefu suala la huduma zinazotumia data kuhusu watumiaji wake kimatangazo n.k, lakini miaka kadhaa baada ya kununuliwa na Facebook inaonekana hilo linabadilika.

Katika taarifa iliyotolewa katika blog yao WhatsApp wametangaza rasmi mwanzo wa utaratibu wa app yao kutuma data mbalimbali kwenda huduma ya Facebook ambapo data hizo zitatumika kwa mambo mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na matangazo.

Baadhi ya data ambazo zitakuwa zinatumwa kwenye mitambo ya Facebook ni pamoja na namba za simu za watumiaji wa huduma ya WhatsApp na inasemekana matumizi ya data hizi ni pamoja nakuboresha mfumo wa marafiki wa Facebook (Friends Recommendations) na pia mfumo wa matangazo.

Wengi wanaona kitu kikubwa zaidi kinachoitajiwa na Facebook ni data za watumiaji wa app hiyo ambazo zinaweza tumika kuboresha matangazo ya mtandao huo, na hapa ndio wengi wanaona kutakuwa na matumizi mabaya ya data za watumiaji wa app hii maarufu.

Huduma shindani kwa WhatsApp ya kuchati ya app ya Telegram inaonekana ndio huduma pekee kwa sasa ambayo watumiaji ambao hawatapendezwa na suala la data zao kutumiwa na mtandao wa Facebook wanaweza kuamia.

Je wewe unajali sana suala la usalama na usiri wa data zako kwenye huduma ya kimtandao na apps?
au unaona kwa kuwa unafurahia huduma basi wawe na uhuru wa kutumia data zako?
"Tujibu kupitia comment hapo chini

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top