Friday, September 16, 2016

Tanzania kushuhudia tukio la kupatwa kwa mwezi leo

Baada ya kushuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kwa jua lililotokea mwanzoni wa mwezi huu, leo usiku Tanzania itashuhudia pia tukio jingine la kupatwa kwa mwezi takribani wiki mbili tuu baada ya tukio la kupatwa kwa jua.

Tukio hili linategemewa kutokea usiku wa leo tarehe 16 huu na linategemewa kuendelea kwa karibu masaa matatu, tukio hili litaweza kushuhudiwa maeneo mengi ya Amerika, Afrika, Asia, Austraria na Ulaya tofauti na lililopita ambalo lilonekana maeneo machache ( hali iliyopelekea baadhi ya watu kufikiri kwamba ni amri ya serikali kwamba tukio hilo limetokea Mbeya ðŸ˜‚😂😂😂😂)


Safari hii tukio ni tofauti yaani ni Mwezi ndio umepatwa hivyo hautahitaji kifaa maalumu kwaajiri ya kushuhudia tukio hilo lakini kama utatumia darubini ama hadubini basi utaweza kuona tukio hili vizuri zaidi.


Tofauti na tukio lililopita ambapo Mwezi ulikuwa katikati ya dunia na Jua safari hii dunia ipo katikati ya mwezi hii inasabisha kivuli cha dunia kiangukie katika mwezi na kuufanya mwezi usiwe angavu kama ilivyo kawaida yake.



Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top