Kuna wakati unakuta unataka kujua ni nani anae angalia
sana akaunti yako ya facebook, iwe wewe ni
admin wa page, group au hata akaunti binafsi nadhani lazima utakua anatamani
sana kujua ninani amekua mfuatiaji mzuri wa profile, group au hata page yako. Basi kama wewe ulikua
unatamani kujua hilo basi usiwe na wasiwasi leo Romanus Technology
tunakuletea njia rahisi sana na salama ya kujua ni nani amekua akitembelea profile, page au group lako mara kwa mara.
Kwa kuanza basi kumbuka ni lazima uwe wewe ndio mwenye
akaunti hiyo ya Facebook kwani bila hivyo hutoweza kufanikisha hatua hizi, kwa
maneno mengine ni kwamba ni lazima uwe
umeingia (ume-login) kwenye akaunti yako hiyo unayotaka kujua nani amekua akitembelea mara kwa mara. Pia ni muhimu
kujua kuwa iii uweze kufanya hatua hizi unatakiwa uwe umeingia (ume-login)
kwenye akaunti yako hiyo kwa kutumia kompyuta iwe ni laptop au desktop.
Baada ya kuhakikisha hayo yote
hapo juu basi twende moja kwa moja tukaangale jinsi ya kuangalia nani anae angalia sana akaunti yako ya facebook. Kwa
kuanza ingia kwenye
akaunti yako ya facebook kisha bofya kwenye profile yako au page au group unalotaka kujua nani amekua anatembelea sana, baada ya hapo
hakikisha page hiyo au akaunti yako
imemaliza kusoma (kuload) vizuri kisha futa hatua hizo hapo chini.
Kwenye Keyboard ya kompyuta yako (laptop au desktop) bofya
vibonyezo Ctrl pamoja na U kwa pamoja yaani (Ctrl+U) au unaweza kutumia Mouse ya kompyuta yako kwa kubofya kibonyezo cha Mouse cha
upande wa kulia (Right Click) kisha chagua sehemu iliyoandikwa view page source hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye page yenye code za akaunti yako. Subiri page hiyo imalize
kusoma (kuload) kisha bofya tena kwenye
keyboard yako Ctrl pamoja na F (Ctrl+F) ukiwa kwenye page hiyo yenye code za akaunti yako.
Baada ya hapo utaona kwenye kioo chako box limefunguka
upande wa kulia juu,
Baada ya hapo utaona namba nyingi zikianza
mbele ya maneno hayo baada ya neno List, namba hizo
zinakuwa na tarakimu 15
copy namba hizo kisha andika www.facebook.com/
kwenye sehemu ya kuandika link
kwenye browser yako kisha weka namba
hizo 15 mbele ya mkato yani www.facebook.com/123456789012345 kisha bofya Enter kwenye keyboard yako.
Baada ya hapo utaona (profile)
akaunti ya mtu ambae ndio anatembelea sana profile page yako kwenye mtandao wa facebook,
kumbuka namba ya kwanza
ndio inayo wakilisha anaetembelea sana kama ukiangalia namba
hizo ziko nyingi inamaanisha zimejipanga kwa mtu wa kwanza mpka wa mwisho.
Kama una tatizo usisite kutujurisha kupitia comment hapo chini na tutakusaidia haraka iwezekanavyo, pia usisahau kuwashirikisha na wenzako (share) kupitia mitandao ya kijamii.
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini