Wednesday, November 2, 2016

Tofauti Kati Ya BLOG na Website


WEB ni nini ? :
Neno WEB ni ufupisho wa neno  WORLD WIDE WEB – si umeona websites nyingine zinaanza na www, basi www ni kifupisho cha World Wide Web. Kwa lugha rahisi WEB ni namna maalum ya kusambaza taarifa kupitia mtandao kwa kuunganisha mawasiliano toka kompyuta tofauti tofauti ulimwenguni.

WEBSITE ni muunganisho wa maneno mawili Web na Site. Wajua neno web nini , basi unganisha na neno Site kama unavyojua neno Site  ni eneo maalum kwa ajili ya shughuli maalum, Basi WEBSITE inamaanisha ni sehemu maalum ambapo habari au taarifa fulani zinapatikana. Mfano kama unataka kusoma status za rafiki zako wa FaceBook basi wajua ni lazima uende katika mtandao wa FACEBOOK. Hivyo FACEBOOK ni SITE kwako maalum kwa  kuangalia taarifa tofauti kutoka kwa watumiaji wake, hivyo FaceBook tunaiita WEBSITE.

Kwa mujibu wa Wikipedia, neno blog ni kifupisho cha neno Web LOG, yaani rekodi au usajili wa taarifa za mara kwa mara ndani ya WEB. Ili kufupisha neno zima WEB BLOG wakaita kwa kifupi BLOG-yaani kutoka neno WEB, tumechukua herufi B, halafu tukaunganisha na neno LOG, hivyo kuwa na BLOG.

Tofauti kati ya blog na website:-
Uandishi :  Kwenye blogs tuna kitu tunaita POSTS ambapo hayo ni maelezo yanayowekwa na mwandishi wa blog mara kwa mara. Hata hivyo websites kwa asili huwa hazibadilishwi taarifa mara kwa mara kama ilivyo blog.

Uhifadhi wa taarifa: Blogs zina mtindo maalum wa kuhifadhi posts toka ya kwanza mpaka ya mwisho kuiandika. Na mara nyingi waweza kuona hifadhi (ARCHIVE) ya posts hizo katika blogs nyingi, hata hivyo websites  nyingi huwa hazina hifadhi ya taarifa zao za siku za nyuma ndani ya websites husika.

Teknolojia: Mtu yoyote yupo huru kuandaa website kwa mtindo anaotaka yeye, tofauti na blogs ambapo tayari teknolojia yake inategemeana na matakwa ya kampuni husika inayotoa huduma ya blogging. Mfano kuna wordpress inao mtindo wake maalum, na blogger nao wana mtindo wao maalum wa jinsi blogs zao zitakavyotokea au jinsi utakavyoziandaa.

Ushirikishwaji wa wasomaji:  Mara nyingi kwenye blogs huwa tuna sehemu ya comments kwa kila post, wakati taarifa za websites nyingi hazina kipengele cha ku comment.

Asasi  nyingi siku hizi zimekuwa zikiambatanisha teknolojia ya blog katika websites zao ili kuendelea kuwa karibu na wateja wao watarajiwa.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top