Tuesday, January 10, 2017

TB 2 – USB Flash Drive yenye ujazo mkubwa zaidi yatambulishwa!


Kampuni kongwe katika utengenezaji wa diski uhifadhi – hard drive na usb flash drive, ya Kingston yatambulisha rasmi USB Flash Drive zenye ujazo mkubwa zaidi.

USB Flash Drive hizo zinazokuja na ujazo wa TB 1 na toleo jingine la TB 2 zitatolewa chini ya familia ya Kingston DataTraveler Ultimate GT, – GT ikimaanisha ‘Generation Terabyte’, yaani kizazi cha terabyte.

USB Flash Drive ya TB 2 itachukua rekodi ya kuwa USB Flash Drive yenye ujazo wa juu zaidi kuwahi kupatikana sokoni.

Flash Drive hizi zimetambulishwa katika maonesho ya bidhaa za elektroniki huko jijini Las Vegas, #CES2017. Zinategemewa kuingia sokoni ifikapo mwezi wa pili mwaka huu ila hadi sasa bei zake bado hazijawekwa wazi ila kwa kiasi kikubwa usitegemee ziwe bei rahisi.

Sifa zingine kwa undani;

  • Ujazo: TB 1/TB 2
  • Kasi: USB 3.1 Gen. 1
  • Urefu na upana: 72mm x 26.94mm x 21mm
  • zitaweza kufanya kazi kwenye programu endeshaji mbalimbali: Windows 10, Windows 8.1, Windows 8, Windows 7 (SP1), Mac OS 10.9.x and above, Linux v.2.6.x and above, Chrome OS

Vipi wewe unadhani unaweza ijaza usb flash hii ya TB 2 kwa vitu gani hasa?


Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top