Saturday, March 18, 2017

Fahamu Umuhimu wa CPU na GPU Katika Simu Yako


Leo nitakuelezea kuhusu umuhimu wa CPU na GPU katika simu yako ya smartphone, ingawa wengi wetu hatufuatilii sana kuhusu vitu hivi ila ni muhimu kupata ufahamu wake haswa katika kufanya simu yako iwe fasta na ukaaji mzuri wa chaji.  

HISTORIA FUPI YA GPU (GRAPHICS PROCESSING UNIT
          Kwanza kabisa hapo mwanzo GPU zilikuwa haziwekwi kwenye simu kabisa, zilikuwa ni kwa ajili ya kompyuta pekee  mpaka mnamo mwaka  2006-2009 ambapo kampuni pekee kipindi hicho iliyokuwa ikihusika kutoa  GPU kwa ajili ya Simu (Qualcom) walisema ni miaka ambayo ilikua migumu sana kwao kwasababu ndio walikua wakianza kuingiza sokoni bidhaa zao na ndipo walipo amua kuomba msaada kwa kampuni ambayo ilikua ikitengeneza GPU za kompyuta iitwayo (AMD) na kwa pamoja wakatengeneza GPU  iitwayo Adreno 130 ambayo ilikuwa ni GPU iliyo fuata baada ya Adreno 120 ambayo ilitengeneezwa na kampuni ya Qualcom pekee na biashara kati ya makampuni mawili iliendelea mpaka Qualcom walipo amua kununua division yote ya Graphics za simu na kuwa mmiliki kamili bila ushirikiano kutoka AMD kwa shilingi $ mil65 na ndipo wakatoa  Adreno 200 na kuifanyia upgrade ikawa Adreno 205 mnamo mwaka 2009. Wala tusisahau makampuni mengine ambayo pia walianza kutoa GPU zao kwa ajili ya simu baada ya kuona soko liko vizuri, hapa sasa kuna makampunia kama PowerVR ambao ndio wapinzani wakuu wa Qualcomm alaf wengine ni kama ARM architecture (mali) na GeForce ULP (Ultra lower Power) (Nvidia)

KAZI KUU YA GPU KATIKA SIMU YAKO 
         Kama inavyo jieleza Graphics processing Unit  ni kifaa ambacho kipo kwenye simu ambacho kazi yake ni kuprocess picha kwa muonekano ulio mzuri na kueleweka  bila kusahau mpangilio wa rangi, na imewekwa special kwaajili ya kufanya kazi hiyo ili kuipa support CPU (central processing unit). GPU na CPU hazitofautiani sana ila GP  haiwezi kufanya kazi nyingine mbali na kazi yake kuu na CPU inaweza kufanya kazi zote mbili ingawa uwezo utapungua kidogo lakini somehow itawez kumanage.

AINA ZA GPU 
      Kuna aina nne za GPU ambazo zinatumiwa katika simu zetu , ila tusichanganye hapa kwamba una graphics ambazo ni Dedicated ambazo zinaweza kutengana na motherboard na hizo motherboard zinakuwa na port muhimu lakini hauto kuta kitu kama hicho kwenye simu za Android  bali kila simu utakapo nunua inakuja na GPU yake ambayo huwezi kubadilsha.

1.Adreno
     Hii ni aina ya GPU ambayo inatengenzwa na kampuni ya Qualcomm  ambayo ni maarufu kwa kiasi kikubwa na imekuwa ikiwekwa kwenye simu kama Moto X zote, Htc one M9,Sony Z3, LG G3,LG G2, Galaxy S7,Galaxy A9,Asus Zenfone nk. Binafsi nimekuwa nikitumia simu nyingi ambazo zina Adreno GPU na kingine ni kwamba hauwezi kutambua utofauti mpaka uwe na simu zenye GPU tofauti. kwa watu wengi wanasema GPU ya mali ni nzuri kuliko zote lakini kwa mimi naona Adreno ndio nzuri.


2.PowerVR
     Hii ni product ya kampuni iitwayo imagination technologies ambao wao waliama kutoka katika utengenezaji wa GPU za laptops na desktops na waka amina kwenye kutoa GPU kwa ajili ya simu na wamefanikiwa sana mpaka kuwafikia wapinzani wao Adreno. simu zilizo na GPU hii ni kama vile Blackberry Q10, LENOVO P90, NOKIA N1, IPHONE 5S nk.

3. MALI

       Hii inatengenezwa na kampun ambayo wanatengeneza CPU za ARM aia hii ya GPU zinasemwa kwamba ndio zinaongoza katika ulimwengu wa android na kwakweli ni GPU nzuri tu sema zina lag sana kwa maelezo ya watu wengi ambao wame experience utumiaji wa simu zenye GPU hii, simu zinazotumia GPU hii ni kama vile   Galaxy s6, S6 edge, Galaxy j1 2016, Galaxy A8, Meizu Pro 5,


4.GeForce ULP

      GeForce ULP (ltra Low Power) aina hii ya processor inatengenezwa na kamuni inaitwa NVIDIA  ambao hawa wanaongoza katika kutengeneza GPU kwaajili ya kompyuta na ndio maana mara nyingi GPU hii inaweka kwenye simtablets sana kuliko GPU nyingine na hii ni kwa sababu y auwezo wake wa kuweza ku process hadi cores 8 na saiz mpaka cores 12. baadhi ya simu ambazo zina tumia GPU hii ni kama vile ASUS VIVO Tab, ASUS NEXUS Tab, SONY EXPERIA Tab S, SAMSUNG GALAXY Tab 8 nk..

Kwahiyo rafiki yangu kama tunavyo ona simu nyingi ambazo  ni maarufu wanapenda kutumia GPU ya kampuni ya qualcomm ingawa kipendwacho na wengi sio kwamba ndio kizuri lakin kwa uwezo wa kampuni hiii na ubunifu mkubwa walio nao nina weza kusema ndio chaguo lililo sahihi haswa kwa sifa mblimbali zinazo tolewa na kampuni hiyo, MALI GPU ni kampuni ambayo inasemekana ina run katika ulimwengu wa android lakin mi naona kwamba  ni kutokana na machaguo binafsi tu. ukiniomba mimi ushauri nitakwambia tafuta simu yenye Qualcomm 

HISTORIA FUPI YA CPU (CENTAL PROCESSING UNIT
       Simu zilianza na matumizi ya processor moja, lakini kadri siku zilivyo zidi kwenda nguvu nyingi zilitumiwa kutengeneza na kudesign processors zenye cores zaidi ya moja katika simu moja ambapo tumeona simu zilianza kuja na core mbili (Dual core) alaf zikaja zenye core nne (Quadcore) baada ya hapo haikutosha na tumeona simu za mwaka 2015 mpaka 2016 zimeanza kuja na processor 6 (Hexacore) na kuna nyingine zimeanza kutoka ambazo zinakuja na cores 8 (Octacores).

Katika Kompyuta CPU, RAM, GPU na HDD zote zina port katika Motherboard, ambayo ina chips za kipekee. Ndani ya smartphone nafasi kubwa imechukuliwa na betri na sehemu kati ya chips tofauti tofauti na hii ni kutokana na kile kinachoitwa System On Chip (SOC) ambayo inatokana na design ya system il iweze kuwasiliana na procesor CORE

Core ni kifaa ambacho kipo ndani ya processor ambacho kazi yake ni kusoma maombi yanayo letwa katika processor na kuyajibu maombi hayo, kwa mfano unataka kupiga picha kwahiyo pale unapo bonyeza ile icon unapeleka maombi na yenyewe ina respond kwa kuifungua hiyo app. 


KAZI KUU YA CPU KATIKA SIMU YAKO 
     processor ndio inafanya kazi ya  kuchukua taarifa na na kusambaza kama utakavyo iamuru, kwa mfano  kurespond  katika vitu mbalimbali ambavyo unataka simu yako ifanye nk, pia inawajibu wa kuwaambia programs ambazo utakua ume install ,kama ni GPS yako au kuliza mlio wa simu..kiufupi processor ni kama brain kwenye simu kwahiyo ina deal na kila operation katika simu.


AINA ZA CPU
   Ziko aina mbalimbali za CPU katika simu zetu  amabazo ni kama zifuatazo..

1.Qualcomm: SnapDragon
     Nchini Marekani, Qualcomm inaongoza  katika jukwaa la kuweka chips zao za Snapdragon SoC (System-on-Chip) kwenye simu za Android, kwa sasa core ya CPU za Snapdragon zinaitwa Krait, na ukiangalia kasi yake haina spidi sana kama ile ya Cortex A15 ambayo ni toleo la ARM, lakin still inaongoza kwa kutumiwa sana na makampuni ya simu, Qualcomm ilikuwa ya kwanza kuanzisha 4G LTE kwa kiwango cha wireless. Hii iliwafanya Qualcomm kutanuka katika soko kiukubwa sana kwa sababu mwisho wa siku LTE ilikuja kuwa ni kitu ambacho ni muhimu kuwa nacho kutokana na feedback za watumiaji kwahiyo kila mtu alipatwa na shauku ya kuwa na hiyo teknolojia.
  

2. MediaTek
        Hizi zinatengenezwa na kampuni inaitwa mediatek au MTK kw kifupi ambapo simu kama Tecno C8 simu nyingi kutoka Huawei pia wanatumia processor hizi  na simu nyingi mno ukiacha Huawei wanapenda sana kutumia processor hizi  mbali na kuwa zinafanya kazi vizuri hata bei zake pia ni rahisi, hivo basi hata ndio  maana simu nyingi za kichina pia aka Fake wanatumia aina hi ya processor. processor ambazo zina nguvu sana kutoka kwa hawa watu ni kama vile Helio X10 (High-End Series of MediaTek), MediaTek MT6735, MediaTek MT6592 nk..

3. Exynos
      Processor  hizi  zinatolewa na kampuni ya samsung na hizi zinafahamka sana kwa kuwa nzuri sana katika games na  multitasking  ingawa kwa upatikanaji wa processor hizi processor ni mdogo sana na mara nyingi zinapatikana katika simu za samsung

4.Tegra
   Aina hii ya processor inatolewa na kampuni ya NVIDIA ambao ni maarufu sana katika utengenezaji wa GPU katika kompyuta na huku wamewea kutoa processor zenye dual core na Quad core  ambapo makampuni mengine uiacha Qualcomm bado wapo kwenye kutoa  Dual core processor.

5.OMAP
   Kampuni iliyo tengheneza processor hizi inaitwa Texas Instruments nalengo lao kuu haswa lilikua ni katika ubora wa ku display video katika quality  vya hali ya juu na pia katika kamera kuhakkisha inatoa picha iliyo na quality nzuri, kwahiyo kama una simu yenye processor hii basi jaribu kulinganisha ubora wa ku display vitu katika kioo chako.

6. PXA
    hizi zinatolewa na kampuni iitwayo Marvell processo na ni ngumu sana kuikuta aina hizi kwenye smartphones za sikuhizi inghawa wao lengo lao kuu wali focus katika kuokoa nguvu nyingi ambazo zinaweza kuwa zinahitajika na processor kwa ajili ya kukamilisha mambo mbalimbali katika simu yako.

Ni vyemma rafiki yangu ukaanza kuangalia maswala ya processor na gpu katika simu unayo taka kununua, hivi ndivyo vinafanya simu yako iwe yamoto au iwe inatunza chaji au iwe fasta haswa processor na kwa upande wa processor nashauri simu zenye processor za Snapdragon (Qualcomm) ambao mbali na kuwa na uwezo wa kusababisha simu yako isiishe chaji kwa haraka pia wana teknolojia mbali mbali.

mfano Fast charging ambayo mimi nimekua niki tumia simu yenye teknolojia hiyo na kwakweli naweza sema inasaidia sana nina weza weka simu yangu kwa dk 15 ikajaa mpaka asilimia 54 hivi ndani ya nusu saa.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top