Friday, April 14, 2017

Namna ya kutafuta sattelite za chaneli bila kubahatisha


Leo nakupa ujuzi huu ili kuweza kufaidi chaneli za FTA kupitia sattelite mbalimbali,
Tuanze na namna ya kuitafuta sattelite kwa uhakika bila kubahatisha pasipo kutumia satelite finder,


Ili kufaidi vizuri kazi au jaribio lako unatakiwa uwe na MPEG 4 DIGITAL RECEIVER ,LNB ZA C BAND NA KU BAND , PAMOJA NA DISH KUANZIA CM 60 NA KUENDELEA KWA LNB YA KU NA DISH KUANZIA FUTI 6 ,8 , 10 na kuendelea KWA LNB YA C BAND.
Hakikisha kila kitu kipo sawa na umejiandaa na majaribio bila kukata tamaa,
Tukianza na namna ya kujua ni wapi satelite inapatikana unatakiwa ujiulize ikiwa IS 906 ni nyuzi 64 Mashariki , (EUTELSAT 36 A ) Dstv ni nyuzi 36 mashariki, Nile sat (ZUKU NA STARTIMES) 7 Mashariki na IS 22 ni nyuzi 72.1 mashariki.


Hapo ukiwa mtafiti utagundua kuwa kumbe kadiri unapozungusha dishi kulia (ukiwa nyuma ya dishi) ndivyo nyuzi zinavyozidi kupanda na kadri unaporudisha dish kushoto (ukiwa nyuma ya dishi) ndivyo nyuzi zinavyozidi kupungua ,
Ila cha muhimu unapotafuta signal ya satelite yoyote usitegemee uone mafanikio kwa haraka haraka inakubidi usome level ya msitari mwekundu ndo upate uhakika kuwa unachokitafuta utakipata muda sio mrefu ,
Kwa mfano unatafuta satelite ya Intelsat 10 unatakiwa kuvizia mida ya jioni jua linapotaka kuzama lengesha lnb ya kwenye dish iangaliane sambamba na jua halafu anza kuzungusha kurudi kushoto itafika sehemu mritari wa level au strength utakataa kupanda zaidi ya 80% au 81% uzilazimishe anza kupandisha na kushusha im sure lazima msitari wa quality utaonekana tu ,

ANGALIZO.
=>HAKIKISHA LNB UMEIFUNGA IMELENGA KATIKATI YA DISH ,
=>MAHALA ULIPOPWEKA DISH KWA MBELE KUSIWE NA VIZUIZI VINAVYOPUNGUZA AU KUKATA SIGNAL (MITI, UKUTA )
=>HAKIKISHA SEHEMU YA ARDHI UNAYOTAKA KUWEKA DISH IPO SAWIA ,

2. kama unataka kusearch satelite kwa kutumia satelite finder, unaweza kuhunt satelite bila hata kuliangalia hilo dishi. na kama mfuko wako upo vizuri zipo hadi zenye built in tv na receiver ukienda site unabeba tu satelite finder yako yenye ukubwa kama simu.




Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top