Leo nikushirikishe juu ya Kutatua tatizo kama kioo cha simu yako ya Kupangusa (Screen touch) hakifanyi kazi. Wakati mwingine hutokea kuwa Kioo cha simu yako hakitoi matokeo pale unapogusa ili kufanya muamala fulani, kama vile Unapogusa ili ufungue mafaili au chochote huwa imeganda tu, au ina mwitikio mdogo isivyo kawaida. Kama haloi hiyo itatokea unashauriwa kufanya Yafuatayo.
1,Safisha kioo cha simu.
Mara nyingi tukiwa katika hali mbalimbali tumekuwa tukitumia simu zetu hali ya kuwa mikono ni michafu na yenye mavumbi. Kioo cha simu kinadaka takataka hizo n kutengeneza layer(tabaka jembamba) ambalo si rahisi kuligundua kwa hali ya kawaida. Hivyo unashauriwa kama unaona kioo cha simu yako kina tatizo kama nililoeleza hapo juu unatakiwa Kutumia kitambaa laini na kilichosafi kusafisha kioo cha simu yako. Jaribu kukandamiza kitambaa kidogo ili kama kuna uchafu uweze kuondolewa.
2.Restart simu yako au zima kisha uiwashe tena kama bado tatizo linaendelea.
Wakati mwingine hutokea kua si kioo (screen) nbali tatizo hutokea katika mfumo wa simu na kuleta matokeo kama hayo, hivyo unashauriwa Urestart(Anzatena kuwasha)n au zima kabisa kisha Uiwashe.
3. Ondoa kikinga kioo (screen cover/screen case)
Kutokana na usalama wakati mwingine mtu huweka kitbaka cha screen ili kuzuia mikwaruzo katika kioo halisi cha simu. Tatizo hutokea pale kikingakioo kinposhindwa kufanya kazi kwa sababu mbalimbali, Hivyo unashauriwa Kutoa kikinga kioo.
ANGALIZO:Ukishatoa hauwezi kukirudishia tena hadi ukaweke kingine.
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini