Apple ID (ile barua pepe inayokufanya uweze kushusha vitu sokoni) imekua gumzo kwa baadhi ya watumiaji wa bidhaa za Apple Inc. Utakuta mtu ana iPhone sema kufungua account ya Apple ni shida kwa sababu inakua inataka taarifa za benki za mtumiaji. Kuna wengine hilo hawaliafiki kwa sababu hawana mpango wa kushusha App ambazo zinauzwa Appstore, Labda wanataka zile za bure tuu. Hata mimi katika iPhone yangu ya kwanza iliniladhimu niwe natumia Apple ID ya mtu mwingine ambae nlikua nimeelewana nae kuhusiana na hilo. Lakini kumbuka ku ‘Share’ vitu kama hivi sio dili, lolote linaweza tokea huwezi jua. Tatizo lingine linakuja pale unapo ‘share’ akaunti ya mtu ambae kaweka taarifa zake za benki, ukiona App nzuri inayouzwa utaishusha? (usinijibu). Kama unataka fungua Akaunti katika vifaa vya Apple bila kuweka taarifa zako za benki fuata maujanja haya
Kwanza kabisa njia rahisi, kabla ya kufungua Apple ID inabidi ufungue parua pepe ya iCloud. iCloud itakua kama ndio njia yako ya kuhifadhi data zako (memory) kama number za simu, taarifa za kalenda, notisi ulizoandika, vimemo na mambo mengine kibao. Uzuri wa iCloud ni kwamba hata pale unapobadilisha simu mfano kutoka kwenye iPhone 4s kwenda kwenye iPhone 5 hauhitaji kuanza kuanza upya kwenye number zako za simu hapa cha kufanya ni kuingiza akaunti ya iCloud uliokua unaitumia katika 4s kweye iPhone 5 na kisha ‘restore’ data zako
Jinsi Ya Kufungua Akaunti Hiyo
- Nenda katika Settings za iPhone Yako
- Tafuta iCloud
- Fungua na bonyeza ‘Get a free Apple ID’
Hapo sasa jaza hiyo fomu vizuri kabisa. kwa kuwa unajiaandikisha kwa mara ya kwanza kabisa ni vyema ukaweka pale mwisho @icloud.com (romanustechnology@icloud.com) usitumie romanustechnology@gmail.com au mengine
Ukishamaliza kujaza fomu hiyo utakua umetengeneza akaunti ya iCloud. Pia unaweza kutuma na kupokea E-mail katika akaunti hiyo hapo hapo kwenye simu yako.
Baada ya kuwa tayari na akaunti ya Icloud, ingia App store kisha fanya kama unadownload app yoyote. ukibofya download tuu kitakuja kiboksi kikidai email na neno siri. hapo jaza ile email ya icloud (romanustechnology@icloud.com) uliofungua juu pamoja na neno siri lake. kitatokea kiboksi tena kikisema ‘This Apple ID has not yet been used with the itunes store please review your account information’ kisha bonyeza review. Itakupeleka katika ukurasa mwingine ambapo utaenda kukubali vigezo na masharti na kujaza taarifa zako za kibenki utakuta machaguo haya Visa, MasterCard, Amex, Discover na None. Hapo chagua ‘None’ kisha utaendelea jaza taarifa muhimu kama jina kamili, umri na jinsia na vinginevyo.
Baada ya kumaliza kujaza fomu hiyo, utakua umefungua akaunti ya iCloud na ya Apple (Apple ID) bila kuweka taarifa zako za kibenki. Anza kutuma na kupokea meseji kutumia iCloud na shusha App uzipendazo za bure katika App Store
Ni muhimu kila mtumiaji wa vifaa vya Apple Inc akawa na Apple ID yake, kwa sababu itamsaidia kutunza hata data zake za muhimu kama number za simu. Haya sasa Romanus Technology imekupa mbinu hii, Tuambie umeipokeaje sehemu ya comment hapo chini pia usisahau kusambaza hii ili kila mtu ajanjaruke.
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini