Kujiingizia kipato/fedha kupitia Internet ni jambo lililoenea Duniani kote. Na hii imedhihirisha Mapinduzi makubwa ya maendeleo ya Sayansi na teknolojia. Vijana,Watu wazima,Wenye ajira na Wasio na ajira Wanafanya kazi Mtandaoni kwa ajili ya kujipatia kipato cha ziada kitakachoweza kukidhi baadhi ya Matumizi yao. Lakini hali hii inaonekana tu katika Nchi zilizoendelea wakati katika nchi Zinazoendelea bado inaonekana watu wamelala. Hata hivyo kwa sasa nchi nyingi Zimeanza kuamka Na Kulipa nguvu jambo hili.
Wengi wanapotajiwa swala la kujiingizia fedha kupitia Internet huona kama ni masihara,na wengine Wakibeza na Kuwakatisha tamaa wale walio tayari kutaka kuthubutu. Niwatoe wasiwasi kwa wale wanaotaka kuingia katika uwanja huu wa kujiingizia fedha kuptia internet. Internet ni sehemu pekee itakayokuwezesha kujiingizia kipato kwa kufanya kazi ukiwa Nyumbani,wakati unaendelea na shughuli zako njingizne.
Unaweza kufanya kazi zaidi ya 100 Mtandaoni na Ukajiingizia kipato Cha nguvu. Kiasi gani unaweza kujiingizia kupitia Internet hutegemea sababu mbalimbali kama vile
1.Aina ya kazi unayofanya.
2.Ubunifu na juhudi katika kazi Unayofanya.
3.Muda,Ni muda kiasi gani unautumia kufanya kazi katika internet.
4.Uimara na iUstadi katika kazi.
5.Elimu juu ya kazi unayoifanya.
Unaweza kujiingizia 100,000/= hadi 5,000,000/= Kwa mwezi,hutegemea na sababu mbalimbali kama zilivyoorodheshwa hapo juu.
Watu Wengi wamekuwa wakifeli Kujiingizia fedha kupitia Internet kutokana na sababu mbalimbali. Zifuatazo ni miongoni mwa sababu zinazowafanya Watu washindwe kujiingizia Fedha kupitia internet.
1.Kukosa elimu sahihi juu ya kujiingizia fedha kupitia Internet.Mengi yanasemwa juu ya kujiingizia kipato/fedha kupitia internet Lakini watu bado wanakosa elimu sahihi ya Kujiingizia fedha kupitia internet.
2.Kukosa Uvumilivu,Kujiingizia kipato cha maana kupitia Inernet ni jambo linalochukua muda.wengi wanashindwa kutokana na kukosa Uvumilivu katika kazi hizi. Inaweza Kuchukua miezi kadhaa na hata mwaka/miaka kabla haujaanza kujiingizia kipato cha maana hii hutegemeana na kazi husika mtu anayoifanya.
NJIA UNAZOWEZA KUTUMIA KUJIINGIZIA KIPATO KUPITIA INTERNET
Zifuatazo ni njia unazoweza kutumia kujiingizia kipato/fedha kupitia Internet. Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kwamba kuna njia/kazi zaidi ya mia moja (100) unazoweza kutumia kujiingizia kipato kupitia Internet, Lakini makla hii itaelezea njia 10 tu za uhakika ambazo unaweza ukazifanya wewe Mtanzania/Mkenya na Ukajiingizia kipato [pasipo tatizo lolote.
ANGALIZO:Hapa hatuelezei njia zitakazokufanya wewe utajirike kupitia internet, bali ni Njia ambazo zitakazokuingizia kipato kinachoweza kukuinua kimaisha. Kutajirika kupitia Internet kunahitaji elimu zaidi.
1.BLOG
Blog ikiwa ni mtandao unaomwezesha mtu kuweka matukio,taarifa na makala mbalimbali ambazo husomwa na watu wengine, inaweza ikatumika kama chnzo cha mapato. Blog ni njia rahisi zaidi ya kujiingizia fedha kupitia Internet. Kwani haiitaji ujuzi mkubwa wa mtandao,Unachotakiwa kufanya ni Kutengeneza blog/kutengenezewa na kisha Kuchagua njia utakayoitumia kujiingizia fedha kupitia blog yako.
HATA HIVYO:Ninaposema blog ni njia rahisi kujiingizia kipato kupitia blog isifikiriwe kuwa ni rahisi kama Kunywa maji bado inahitaji Muda,kujituma na Ubunifu ili kufanikisha hilo.
2.Kuwa mwandishi wa Vitabu Mtandaoni.
Miongoni mwa vikwazo vinavyowazuia Waandishi wengi kutimiza ndoto zao ni UCHAPISHAJI WA VITABU.Kutokana na Ukosefu wa gharama za Uchapishaji wa vitabu,Watu wenye fani hii ya uandishi wamekuwa wakiishia njiani. Internet imefungua Milango wazi kwa Waandishi,Unaweza kuandika Vitabu na Ukaviuza mtandaoni kwa na kujiingizia kipato. Haijalishi ni aina gani ya vitabu unaandika iwe Vya hadithi,simulizi mabalimbali, Masomo au Mafunzo bado utapata Wasomaji Wako mtandaoni na utajiingizia kipato kupitia kazi hiyo hapahapa Tanzania,Kenya au Nchi nyingine kama Utaandika kwa lugha ya kiingereza. Unaweza kuandika Vitabu na ukavitangaza katika Mitandao mbalimbali itakayokusaidia kupata wateja kama Vile Bookstz,Jamiiforums,OLX,Kupatana.com na mingine mingi.
3.Fundisha Mtandaoni.
Kama una maarifa yoyote na unataka kuyafikisha kwa Watu kwa na huku wakikulipa gharama kidogo,basi internet inakuwezesha kutimiza lengo hilo.Unaweza ukapangilia Maarifa yako katika mfumo mzuri na unaoeleweka na kuanza kutoa mafunzo hayo.Tafuta njia ya kufikisha mafunzo hayo kwa wahusika.
Unaweza kutumia Blog ukaweka Mafunzo yako na Ukaifanya Blog yako kuwa ya kulipia,Yaani mtu hawezi kusoma yaliyomo hadi alipie ada ya mafunzo husika.hii ni njia nzuri kama utakuwa na maarifa ya maana ambayo utawashawishi watu Wajiunge na mafunzo hayo.
4.Anzisha Magazeti ya Mtandaoni(Online Magazine)
Kama Ungependa kufikisha Taarifa kwa watu kupitia magazeti,Tumia njia hii ya Mtandaoni Unayoweza kufikisha taarifa kwa haraka.Utaweka Ulinzi na hivyo ili mtu aweze kusoma Magazeti yako atatakiwa alipie ndipo aunganishwe na huduma hiyo.Ukiwa Mbunifu katika hilo unaweza kujiingizia kipato cha Nguvu kupitia blog.
Njia zote zilizoelezewa katika makala hii ni za uhakika na zinazoweza kukuingizia kipato kupitia internet.
MAKALA HII ITAKUWA IKIONGEZWA VITU VIPYA MARA KWA MARA HIVYO UNASHAURIWA KUIPITIA KILA BAADA YA SIKU KADHAA.
Kwa msaada wowote usisite kuuliza kupitia comment hapo chini…..
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini