Friday, October 21, 2016

Jinsi Ya Kujitoa Kwenye Group la WhatsApp Na kulifuta Kwa Siri


WhatsApp licha ya kutuleta kwake karibu lakini bado kuna vitu vingine vinaboa katika mtandao huo kama ma’Group’ yasiyoeleweka. Je ufanye nini?

Utakuta ndani ya WhatsApp ‘Group’ moja lina watu kibao na wanaongea vitu tofauti tofauti na kibaya zaidi wawe wameku Add tuu bila idhini yako. Hii sasa haitakuboa bali itakukasirisha. Au kama uko kwenye ‘Group’ ambalo sio zuri ki maadili labda vitu vinatumwa na kupokewa na watu wa kundi hilo havina maadili hapo vinaweza kukuharibia siku yako.

🙂 hii ni jinsi ya kujitoa kwenye group la WhatsApp bila watu kufahamu – na huku ukilisambaratisha group ilo kabisa"

 Sasa basi kama unataka kujitoa katika Group ndani ya Mtandao wa WhatsApp bila ya watu wengine katika lile ‘Group’ kujua kama umejitoa, kuna njia spesheli ya kufanya hivyo. Katika kutumia njia hii pia utalazimika kuliharibu ‘Group’ kabisa kwani baada ya wewe kujitoa kwa njia hii, ‘Group’ halitaweza kufanya kazi kabisa (litakuwa limeharibika)

Tuifahamu Njia Hiyo

  • Cha kwanza kabisa itakubidi utumie huduma ya WhatsApp ya kwenye mtandao yaani WhatsApp Web
  • Romanus Technology inashauri utumie kivinjari cha Google Chrome (vingine vina hatihati ya kukwama kuliwezesha hili)
  • Fungua Simu yako na ingia katika WhatsApp. Ukiwa kule nenda eneo la ‘Settings’ na kisha chagua WhatsApp Web kisha skani kodi ya QR katika kivinjari cha kompyuta yako kwa kutumia simu yako. Kwa kufanya hivi unaweza ukatumia WhatsApp katika kompyuta yako
  • Ukiwa unatumia WhatsApp katika Mtandao wa kompyuta (web) fungua ‘Group’ ambalo unataka kujitoa na kulifunga. Anza kuandika emoji nyingi kadri uwezavyo ili zifike takribani 3000 katika ule uwanja wa meseji. Kwa njia rahisi ili kulifanikisha hili inakubidi uwe una kopi na kupesti taaratibu.

  • Ukishapata emoji zako takribani 3000 – 4000 (utajua tuu kwani meseji yako itakua ni ndefu sana) bofya ‘Enter’ ili kutuma meseji hiyo. Na hapa usiwe na haraka sana subiria mpaka Chrome iweze kutuma meseji hiyo na subiri mpaka meseji hiyo ipate tiki moja ikiwa na maana kwamba umetoka(imetumwa).
  • Baada ya kufanya hivyo sasa unaweza ukafunga WhatsApp Web yako na ukienda katika WhatsApp kwa kutumia simu yako, wewe pamoja na watumiaji wengine wa hilo ‘Group’ watapata meseji ifuatayo “WhatsApp isn’t responding”
ujumbe ukisema whatsapp isn't responding
Baada ya hapo hilo ‘Group’ la WhatsApp halitawezwa kutumika hata kwa mtu mmoja kati ya wale ambao walikuwa katika ‘Group’ hilo. Hapa kila mtu atalazimishwa kujitoa katika ‘Group’ hilo. Na kizuri ni kwamba hawaatamjua mchawi ni nani kwani kutakuwa hakuna ushahidi juu ya jambo hili. Wengi watajua ya kuwa labda ni matatizo ya kiufundi kutoka kwa mtandao wa WhatsApp wenyewe.
Lingine la muhimu ni kwamba njia hii sio ya kutumia kwa mzaha. Maana wengine wanaweza wakachukulia kama kamchezo flani. Kabla ya kuifanya fikiria kwanza

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top