Hii ni njia nzuri sana kuwakomesha wale watu wanaopenda kuangia kwenye gallery na kuanza kuangalia picha zako bila ridhaa yako. Muda mwingine hata wazazi hupenda kushika simu na kuanza kuangalia picha kwenye gallery na muda mwingine unakuta una video na picha zenye utata na hupendi mzazi wako azione. Sasa njia ipo ya kuzuia hayo mambo kama hayo yasikupate
JINSI YA KUZUIA BAADHI YA PICHA NA VIDEO ZISIONEKANE KWENYE GALLERY
Download Es Explorer kutoka kwenye play store au tumia link chini kuweza ku download
http://www.apkmirror.com/wp-content/themes/APKMirror/download.php?id=53753
http://www.apkmirror.com/wp-content/themes/APKMirror/download.php?id=53753
STEP 1
Fungua Es file Explorer app kisha tengeneza folder halafu nenda kaamishe picha zako zote pamoja na video ambazo hupendi mtu yeyote azione pale anapofungua gallery yakoSTEP 2
Baada ya kuamisha picha na video zote, fungua tena hilo folder ulilotengeza kwa kutumia Es File Explorer kisha bonyeza vidoti vitatu juu kulia kama picha chini inavyo onekanaSTEP 3
Bonyeza kipengele kinachosema New kisha bonyeza kipengele kinachosema file na kisha andika hili neno .nomedia kama picha inavyo onekana chini halafu bonyeza okHongera, umeweza kuzuia..
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini