Wednesday, November 16, 2016

Jinsi ya kupiga simu za video katika WhatsApp.

Hatimaye mtandao wa WhatsApp umeanza kutoa huduma za simu za video kwa wateja wake, katika tangazo ambalo mtandao huo umelitoa WhatsApp inasema inataka huduma hii mpya iweze kuwafikia watumiaji wote wa simu tofauti na mitandao mingine ambayo inatoa huduma hiyo.
Huduma hii inafanyaje kazi!?
Kwa kila mtumiaji wa App hii ya WhatsApp atahitaji kupakua na kusanikisha toleo jipya la app kisha baada ya hapo ili kupiga simu ya video utafuata utaratibu ule ule wa kupiga simu ya kawaida ila utakapo taka kupiga simu itakuuliza kama unataka kupiga simu ya kawaida ama ya video.
Bila shaka muonekano wa video katika simu ya video ni tofauti kwa kila aina ya simu na Os husika lakini kiujumla huduma hii itapatikana kwa aina zote za simu na aina zote za OS, pengine hii ni moja ya faida za WhatsApp ukilinganisha na huduma kama Facetime ambayo ipo katika iOS tuu.

Hatua za kupiga video call katika whatsapp
  1. Fungua chati

2. Bofya kitufe cha kupigia simu


3. Chagua Video Call

Hapo utaweza kufurahia huduma ya Video call katika whatsapp.

Tungependa kusikia maoni yako kuhusu huduma za simu za video je!? unazitumia na kama jibu lako ni ndiyo unatumia huduma zipi zaidi?



Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...