App hii itafanyaje kazi!?
App hii amabayo kimsingi itakuruhusu kuchagua namba kadhaa za simu ambazo zitapewa uwezo wa kupata location yako katika simu, unaweza kuamua kusambaza location yako ama moja kati ya namba ulizoweka kama trusted contact inaweza kuomba taarifa za mahali ulipo na kupewa (iwapo hautazuia ombi hilo).
App hii inaweza kutumika katika nyakati mbili kama ifuatavyo
- Ukiwa katika matatizo
Kwa mfano upo katika jengo la ofisi yenu na kuna moto umeshindwa kutoka unaweza kusambaza location yako hii itawasaidia ndugu zako kuweza kusaidia ukaokolewa kwa haraka zaidi.
- Ukipotea mitaa
Mara nyingi tunaenda mitaa ambayo hatuifahamu vizuri na kupotea sio jambo geni ( labda kama unapotea mtaa huo huo kila siku ) ukijikuta katika mtaa umepotea na unaona noma kuonekana mshamba kwa kuuliza basi unaweza kumtumia ramani ya ulipo mtu anayeifahamu mitaa vizuri kisha yeye atakuelekeza.
Hii ni app kwaajiri ya kina nani hasa?
Hii app inatabiriwa kuwa itapendwa na wazazi ambao wangependa kufuatilia nyendo za watoto wao, pia kwa wapenzi ambao kidogo wana wivu na wenza wao ama ambao wanahisi wapenzi wao sio waaminifu ( kaeni tayari wenye michepuko, wake kwa waume )
Ili kufanya kazi vizuri app hii basi inahitaji wewe na hao watu unataka uweunapata taarifa zao muwe mmeipakua na kuiweka app hii katika simu zenu.
Iwapo simu itazima kwa kuishiwa betri ama kukosekana mtandao ulipo basi app hii itatuma taarifa za mahali ulipokuwepo mwisho kabla simu haijazima.
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini