Saturday, December 31, 2016

WhatsApp kuruhusu kufuta ujumbe uliokwishatumwa


Je umewahi tuma ujumbe flani na ndani ya dakika chache tayari unagundua umefanya hivyo kimakosa? Whatsapp kuja na uwezo wa kufuta ujumbe uliokwishatumwa.


Katika toleo la beta la simu za iOS (lililokwenye mtengenezo) kwa sasa la app hiyo maarufu uwezo huo unaonekana katika eneo la ‘settings’.
Kikubwa ni kwamba utaweza kufanya hivyo kama tuu mtumiaji mwingine bado hajausoma ujumbe huo. Kama ukishasomwa basi hautaweza ufuta tena.

Uwezo huo utafanyaje kazi?
Ukishatuma ujumbe basi utaweza kubofya na kuendelea kushikilia kwenye ujumbe huo ulioutuma na utapata mapendekezo mawili. ‘Edit’ yaana fanya maboresho au ufute – ‘revoke’.


Hadi sasa WhatsApp wenyewe hawajatoa taarifa rasmi juu ya lini uwezo huo utakuja kwa watumiaji wote wa WhatsApp. Kikubwa ni kwamba ni kitu ambacho tukitegemee kuja katika toleo lolote jipya kwa sasa.
RomaTech ndiyo mtandao wako namba moja katika masuala yote ya teknolojia, Tembelea kila siku.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...