Monday, December 5, 2016

WhatsApp kutopatikana tena kwa Mamilioni ya simu! Fahamu kama simu yako Imenusurika

kutopatikana tena kwa mamilioni ya simu za Android na iOS ifikapo mwaka 2017. Uamuzi wa WhatsApp umetokana na simu hizo kuwekwa kwenye kundi la simu za zamani sana na hivyo kutohimili mambo mapya yanayowekwa kwenye app hiyo.
WhatsApp wanaomilikiwa na Facebook, wamesema wataanza taratibu kuacha kutuma masasisho (updates) kwa mamilioni ya simu duniani kote ifikapo Januari mwaka huu.

Kundi la kwanza litakaloathirika ni simu za Windows, Android na iOS, na pia kufikia mwezi wa sita mwaka 2017 simu zitakazoathirika na uamuzi huo zitaongezeka, wataongeza zingine za BlackBerry, Nokia S40 na Nokia Symbian S60.
Kupitia blog yao wamesema sababu kuu ni kwamba simu hizi za zamani hazina uwezo wa kuendana na teknolojia za kisasa zinazoletwa ndani ya matoleo ya kisasa ya WhatsApp.
App ya WhatsApp ilianza kupatikana rasmi mwaka 2009, na hadi sasa inawatumiaji zaidi ya bilioni 1. Mwaka 2009 wakata wanaanza zaidi ya asilimia 70 ya simu ambazo app hii ilikuwa inafanya kazi ilikuwa ni za Nokia na BlackBerry.
Ni simu gani zitaathirika?
Kwa simu za Android inajumuisha simu zote zinazotumia toleo la Android 2.1 na Android 2.2. Kwa simu za Windows ni simu zote zinazotumia toleo la Windows 7. Kwa iPhone ni simu zinazotumia iOS 6, kama iPhone yako inaruhusu kusasisha (upgrade) basi fanya hivyo kwenda toleo jipya – ila kwa iPhone 3GS ambayo iOS 6 ndio mwisho basi kwao WhatsApp ndio ‘bye bye’.
Wenye muda hadi Juni 2017: BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60.
‘Uamuzi huu ni mgumu sana kwa sisi kuuchukua ila ni uamuzi sahihi ili kuweza kuwapatia watu njia bora zaidi ya kuwasiliana na marafiki, familia na wapendwa wao kwa kutumia WhatsApp’ – maneno yaliyosemwa na WhatsApp

Vipi umeuchukuliaje uamuzi huu? Je simu yako ipo salama? Tujibu kwenye uwanja wa comments hapo chini


Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...