Wednesday, January 25, 2017

Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni


ebay ni sehemu ambayo wauzaji(Seller) na wanunuaji(Buyer) wanakutana Muuzaji(Seller) anajiunga kwa kufungua Account ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa popote pale Duniani
Mnunuzi(Buyer) anajiunga kwa kufungua Account ebay popote alipo Duniani kisha anachagua bidhaa nayoitaka iliyotangazwa na Muuzaji(Seller) ana inunua online.


Ili kukamilisha zoezi la malipo na kuuziana bila kuibiana ndio sasa anaingia Pay pal,

Pay Pal ni njia ya malipo ambapo mtu yeyote anajiunga ili mradi awe ni mteja wa Bank inayotoa Card za Master au Visa Card
Kibongo Bongo CRDB wapo vizuri, baada ya kufungua Acc na kupewa Master/Visa Card yako unarudi tena CRDB kuomba wai link Master/Visa Card yako iweze kufanya online Transaction kwa kujaza form maalumu then you're done

Baada ya kadi yako kuwa Linked unajiunga kwa kufungua Acc Pay Pal kwa maana ya kwamba unawapa details za Account yako na kuwapa ruhusa kutoa pesa kwenye account unapo waomba kufanya hivyo

Jinsi ebay na Pay Pal wanavyofanya kukamilisha mpango mzima
ebay ni kama soko ambalo watu hawaonani, mmoja yupo Hong Kong anauza iphone mwaingine Yupo Manzese Tz anataka kuinunua lakini wanakuta online through ebay. so huwezi ukamtumia tu mtu hela kwenye acc ya bank maana anaweza kuingia mitini na asiwepo wa kufuatilia


Sasa wanapotaka kulipana Pay Pal anaingia katikati kama bima wa malipo kwa kuhakikisha anamjua vyema Muuzaji(Seller) ambaye ndio mlipwaji

Mlipaji aka Mnunuzi(Buyer) aliyeko Manzese hamlipi direct mlipwaji aka Muuzaji(Seller) aliyeko Hong Kong,
Anachofanya Mnunuzi(Buyer) anampa ruhusa Pay Pal atoe pesa kwenye Acc yake ya bank kutumia Master/Visa kisha amlipe Muuzaji(Seller)

Kwakuwa Pay Pal anakuwa amechukua dhamana ya malipo ya mauziano yenu anawajibika kuhakikisha Muuzaji(Seller) ana bidhaa kweli anayouza na anaaminika atatuma kwa Mnunuzi(Buyer) kile alicho tangaza,....Fail to do so basi Pay Pal atawajibika kumrudishia Mnunuzi(Buyer) pesa yake, na baada ya hapo Pay Pal kushirikiana na ebay ndio watao mtafuta na kumbana Muuzaji(Seller) kwa utapeli alioufanya lakini wewe utakuwa tayari umerudishiwa pesa yako iwapo watajiridhisha kuna uvunjifu wa makubaliano.


Siku hizi biashara zimerahisishwa sana na maendeleo ya mtandao wa intaneti unaowezesha watu kuuza na kununua vitu na huduma kupitia mtandao. Kwa sababu ya maendeleo haya, mara nyingi tunapokuwa tunatumia mtandao wa internet tunakutana na vitu mbali vizuri kama vile software, vitabu, nguo, saa, magari au hata kozi ya kusoma kwenye mtandano.

Mara nyingi vitu hivi huwa na bei nzuri sana ambayo huvutia kununua. Shida kubwa na yenye mantiki inayojitokeza ni usalama wa pesa zetu na akaunti zetu za benki tunapofanya manunuzi kwenye mtandao. Mimi binafsi ni mnunuaji wa kwenye mtandao hivyo nitakwenda kuelezea vitu vya muhimu vya kufanya kabla hujatoa namba ya kadi yako ya benki kwenye matandao.

1. Tafuta Debit card au Credit card

Debit card ni kadi inayokuwezesha kununua vitu kwenye mtandao kwa kutumia pesa iliyo kwenye akaunti yako ya benki. Na Credit card inakuwezesha kununua kwa kukopa kwenye benki unayotumia halafu wanakukata kidogokidgo kwenye mshahara wako au namna yoyote ambayo mtakubaliana na benki. Kadi hizi ni kama Tembo card visa na Tembo card master card za CRDB Bank;

benki zingine kama NBC, Stanbic Bank na BARCLAYS Bank pia zinatoa Kadi Za namna hiyo. Baada ya kupata kadi yako unatakiwa uende kwenye benki yako wakairuhusu kuweza kufanya manunuzi kwenye mtandao.

2. Jiunge na tovuti ya Paypal.

Paypal ni tovuti inayoongoza duniani kwa kusimia malipo ya kwenye mtandao. Kazi yake kubwa ni kutunza taarifa zako muhimu za benki ili wamachinga wa kwenye mtandao wasizizoee hovyo. Hivyo basi ukitumia paypal, unasajili na kuweka namba yako ya visa au master card.

Baada ya hapo unaweza kuweka pesa kwenye account ya paypal au ukaziacha kwenye akaunti yako ya benki. Unapofanya manunuzi Yule muuzaji anapewa pesa na Paypal sio wewe moja kwa moja ili kulinda taarifa zako za benki.

3. Nunua kwenye tovuti iliyo na mfumo wa kutuma taarifa zako kwa usalama.


Kwa ajili ya usalama kuna teknologia inaitwa SSL(Secure Socket Layer). SSL inafanya kazi ya kusafirisha taarifa zako katika hali ya mkanganyiko ili mtu yoyote mhalifu asiweze kuzielewa, zikifika zianaundwa tena ili muuzaji aweze kuzielewa.

Teknologia hii inatumika pia kutuma email, blackberry wakiwa ni vinara wa kutunia teknologia hii. Ili kujua kama tovuti inatumia hii teknologia utaona alama ya kufuli kwenye anuani ya tovuti husika ikishafunguka. Angalia kwenye sehemu ya kuandikia anuani, kushoto au kulia.

4. Tumia tovuti inayoaminika

Unaponunua kitu kwenye mtandao kwanza kabisa hakikisha hiyo tovuti inafahamika, kama haifahamiki hakikisha kuwa imethibishwa na na mashirika yakuhalalisha biashara za kwenye mtandao kama BBB (Better Business Bureau), utaona nembo ya haya mashirika chini kwenye tovuti ya muuzaji.

5. Nunua kwa muuzaji anayekubaliwa na weteja wengi.
Utajuaje kama muuzaji anakubalika sokoni na anauzoefu wa kuuza vitu kwenye mtandao? Rahisi! Kwa mfanounataka kununua saa Ebay au kitabu cha electrniki (PDF) kwenye Amazon, chini ya hiyo bidhaa iliyoichagua utaona maoni ya watu walionunua kabla yako.

Ni vizuri ukatumia muda wa kutosha kusoma maoni ya waru wengi kabla hujaendelea za zoezi la manunuzi. Njia nyingine ya kupata maoni ya watu ni kutumia tovuti kama Yelp, Google+, Yahoo directory au Yellow pages iwapo muuazaji atakuwa amejiunga nazo.

6. Chagua namna ya kutumiwa mzigo wako.

Unatakiwa kuchagua namna kutumiwa mzigo wako ambayo itakuwa rahisi kwako kuupata. Gharama za kutuma mzigo zitaoneshwa pale kwenye mtandao na muda wa kufika kwa kila gharama. Kwa Tanzania unaweza kutumia DHL, UPS au shirika lolote unaloliamini.

7. Hakikisha muuzaji anahudumia eneo ulilopo.

Baadi ya wauzaji huchagua nchi au miji wanayoweza kutuma mizigo na wengine huuza dunia nzima. Taarifa hizi huwekwa chini ya bidhaa unayotaka kununua , hii itakusaidia kuokoa muda kuondoa usumbufu usio wa lazima.


Enjoy.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...