Thursday, February 23, 2017

Fanya Yafuatayo Ili Kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ kwa kushirikiana na watoa huduma za simu nchini wameanzisha huduma ambayo itamuwezesha mtumiaji wa simu kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba, huduma hiyo inatarajiwa kuanza March mosi Mwaka huu.

Kaimu Naibu Mkurugenzi maendeleo ya TEHAMA kutoka TCRA, Mhandisi Nehemia Mwenisongole amefafanua baadhi ya mambo katika zoezi la kuhama mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu.

mambo hayo ni kama ifuatavyo:-

"TCRA na watoa huduma wamekuja na huduma inayomuwezesha mtumiaji wa simu kuhama mtandao bila kubadili namba ya simu, Ukihama mtandao unahama na namba ileile ikiwamo zile za mwanzoni zinazotambulisha mtandao uliopo, Unapotaka kuhama mtandao bila kubadili namba ya simu unatakiwa uende kwa mtoa huduma wa mtandao unaotaka kuhamia.

Utakapoenda kwa mtoa huduma ambaye unataka kuhamia utajaza fomu, atachukua taarifa zako na atatuma lile ombi unakohama, Akishatuma taarifa kwa mtoa huduma ambako unahama, kwa kutumia simu yako utatuma ujumbe wenye neno HAMA kwenda 15080.

Ombi lako la kuhama litakapokubalika, mtoa huduma atakupatia line ya simu mpya yenye namba ileile, Zoezi la kuhama mtandao wa simu kwa namba ileile ni la hiari, Kama kila kitu kipo sawa kwamba anayetaka kuhama mtandao hana tatizo lolote, zoezi litatumia chini ya dakika 15.

Ukihama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine, kule ulikohamia unatakiwa ukae siku 30, baada ya siku 30 ndio unaruhusiwa kuhama, Endapo utapiga simu kwenye namba ya mtu ambaye ameshahamia mtandao mwingine, utapata ishara ya milio miwili, Huduma ya kuhama mtandao wa simu kwa namba ileile ipo nchi nyingi lakini ni kwa ajili ya nchi husika haivuki mipaka.

Kule unakohama haruhusiwi kuitoa namba ambayo umehama nayo, zikipita siku 90 haitumiki, ulikohamia watairudisha, Katika zoezi la kuhama, zile huduma zote zinazohusiana na kifedha zitasimamishwa, kabla hujahama hakikisha fedha zako umezitoa, Zoezi la kuhama mtandao ni bure ila mtoa huduma atalazimika kukupatia laini mpya, kukutoza fedha ya laini itategemea na mtoa huduma.

Zoezi la kuhama mtandao ni bure ila mtoa huduma atalazimika kukupatia laini mpya, kukutoza fedha ya laini itategemea na mtoa huduma.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...