1. IZIME SIMU YAKO UNAPOICHAJI
Ukizima simu unafanya shughuli zote zilizomo ndani ya simu zisimame yaan zile applications zinazofanya kazi chini kwa chini. Kwa hiyo matumizi ya betri yanakuwa 0% na hivyo kuifanya simu yako ijae chaji haraka
2. ZIMA DATA,BLUETOOTH,WIFI NA GPS
Hivyo vyote vikiwa ON au kimojawapo, hutumia nguvu betri kwa asilimia kubwa.Kwa mfano kama ukiwasha data utaendelea kupokea notifications mbalimbali mfano jumbe za Gmail au Whatsapp Hivyo ukizima unaipunguzia simu mzigo.Hiyo itakuwezesha kuichaji simu yako kwa haraka zaidi kwani shughuli zote za kutumia data zitakua OFF.
3.TUMIA KUCHAJIA CHAJA ORIGINAL
Hizi simu huwa zinaletwa na vifaa vyake original kama chaja, Kwahiyo jitahidi unaponunua simu ununue na chaja yake ambayo imetengenezwa maalum kwa ajili ya hiyo simu. Usipende kutumia chaja zingine ambazo pengine ni bei rahisi na mara nyingi huwa zinaifanya simu inajaa taratibu sana na pengine haijai kabisa hata unachaji siku nzima.
4. USIICHAJI SIMU YAKO KWA KUTUMIA COMPUTER, DEKI AU LAPTOP
Najua utashangaa pengine kwa kuwa umezoea kuona watu wanachaji simu zao kwenye kompyuta,deki za dvd au laptop. Ukweli ni kwamba, yale matundu yote ya USB (USB ports) yamewekwa mahususi kuweza kupitisha umeme kiasi cha 5V @ 0.5 amp. Kwahiyo hicho ni nusu ya kiwango cha umeme unaotakiwa kuchaji simu, Maana yake ni kwamba simu yako itakuwa inaingiza chaji kwa nusu spidi ya ile ya kawaida kwasababu umeme unaoingia toka kwenye kompyuta ni nusu ya ule unaotakiwa.Na hii kwa namna moja ama nyingine inaua simu. Hivyo nakushauri utumie chaji za kawaida ambazo zimetengenezwa maalum kwa simu.
5. USITUMIE SIMU YAKO WAKATI UNACHAJI
Pengine umeambiwa mara kadhaa au umesikia kuwa simu huwa zinalipuka ukiitumia huku unachaji. Ukweli ni kwamba haijathibitishwa, ila inategemea na ubora wa vifaa unavyotumia. Umeme ni umeme, kama vifaa unavyotumia ni fake, basi lolote linaweza kutokea. Sasa ukiwa unatumia simu huku unachaji itakuwa inaingiza umeme kiasi na kutoa kiasi. Kwahiyo utatumia muda mrefu kuifanya simu yako ijae. Na kwa tahadhari tu usiongee na mtu katika simu huku simu iko chaji.
Hizo ni baadhi ya njia ya kuifanya simu yako ijae chaji haraka. Hakika utafurahia simu yako kwa kukaa na chaji kama ukiwa umekubali kufuata njia hizi.
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini