Thursday, February 16, 2017

Njia rahisi ya kuficha mambo yako kwenye simu


kama unamiliki smartphone, nataka nikupe ujanja tofauti tofauti ambao unaweza kutumia ili kulinda mambo yako yasivurugike hata kama mtu atakaa na simu yako mwaka mzima.

1.Kutumia password mbili kwenye simu moja wakati wa login.
Asilimia kubwa ya simu za kisasa zina option mbili wakati wa ku-login yani unaweza kutumia USER or GUEST password.

Sasa ishu iko hivi kwenye settings za simu yako sehemu ambayo imeandikwa security (mfano simu za Huawei) kuna sehemu imeandikwa "privacy protection" ukiingia hapo utapata option ya kuset hizo password mbili user na guest password,

hapo pia utapata nafasi ya kuweka vitu kama vifuatavyo.
(a) private contacts
(b) private album
(c) Private application

Kwahiyo sasa hapo unaweza kuchagua ni namba gani za simu ziwe private, kwamaana kwamba mtu atakaye login na GUEST password hawezi kuziona hizo namba kwenye contacts list, call log, na hata akiangalia kwenye sms hawezi kuona massage za zile namba ambazo ni private.



lakini kitu kizuri zaidi ni kwamba hata kama hiyo simu mtu atakaa nayo na namba yako ambayo ni private ikapiga au kutuma sms haiwezi kuingia mpaka uweke USER password ndiyo message zitaingia.

Vivyo hivyo kwenye private album mtu akitumia guest password hawezi kuona zile private albums, na hivyo pia inahusika kwenye private application.




2.Kama unataka mtu asitumie application yeyote ambayo inatumia internet kwenye simu yako fanya hivi.

Nenda kwenye settings za simu yako then nenda sehemu imeandikwa "networked app" nenda kwenye application husika halafu switch off hapo kwenye mobile na wifi,ukifanya hivyo hata kama mtu akae na simu yako mwaka mzima hawezi kupata sms WhatsApp au Facebook nk.hata kama bundle ikiwa imewashwa 4G 




3. Kwa watumiaji wa Huawei nenda kwenye phone manager then utaona sehemu imeandikwa "harassment filter" click then utaona option mbali mbali kama inavyoonekana hapo chini



Kuna sehemu hapo imeandikwa "interception rule" ukiingia hapo utaona hizo option tatu yani, blacklist interception hii inasaidia kuzuia namba ambazo umeziweka black list,kitu kingine ambacho kinaonekana hapo ni "stranger interception" hii inasaidia kuzuia namba yeyote ngeni na mwisho ni "uknown number interception" inasaidia kuzuia namba ambazo hazina code ya mtandao wowote hapa Tanzania

Kuna sehemu imeandikwa "interception remainder" hii inakupa option ya kutuma or kutotuma notification kwenye screen pale mtu ambaye simu yake imezuiwa anapopiga simu au kutuma sms,ukiwek off hapo hata mtu akiwa ameshika simu yako hawezi kujua kama sms au simu imeingia.

Mwisho.
Njia hizo utaweza kuzitumia kwa mtu ambaye haijui simu vizuri kama ilivyo kwa asilimia kubwa ya wanawake ambavyo hawajua kuchokonoa simu zao.

NB: Kwa namna yeyote ile sitahusika na mambo yeyote ambayo yatakukuta baada ya kusoma na kuamua kufanyia kazi maudhui ya hii makala.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...