Friday, February 24, 2017

WhatsApp yaleta status zenye mtindo wa Snapchat

WhatsApp inafanya maboresho makubwa ya kimuundo tangu kuanzishwa kwake miaka takribani nane iliyopita, kuanzia sasa watumiaji wa mtandao huo sasa wataweza kuweka status ambazo zinajifuta baada ya masaa 24.

Je toleo hili limekuja na nini kipya?

Kwa ufupi toleo jipya la WhatsApp limeleta kipengere kipya ambacho watumiaji wataweza kusambaza video, picha, au GIF. 
hii ndio namna ambayo mtandao wa Snapchat umekuwa ukifanya kazi, tayari Instagram walikwishaiga mtindo huu wa ‘stories’ hivyo WhatsApp ni kampuni ya pili inayomilikiwa na Facebook kuiga mtindo huu.


Je maboresho haya yana maana gani hasa?

Kibiashara kampuni ya WhatsApp tofauti na Facebook na Instagram bado haija fungua milango yake kwa matangazo. Hivi karibuni vyanzo viliwanukuu wamiliki wa mtandao huo wakisema kwamba wanatafuta namna ambayo wataweza kuleta matangazo katika app hii, wengi wanaamini maboresho haya yanalenga kuleta matangazo katika app hii pendwa.
Ikumbukwe kwamba mitandao kama Twitter tayari ipo katika matatizo kutokana na kushindwa kutengeneza mapato ya kutosha, maboresho haya ni wazi yanalenga katika kuifanya app hii kutengeneza pesa zaidi.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...