Karibu ndugu msomaji, na leo tutakwenda kuzungumzia maana ya megapixels katika Simu ,Digital camera, DSLR au laptop.
Nini maana ya MEGAPIXELS?
kiufupi neno megapixel lina ashiria million pixels ikimaanisha hizo pixels zina uhidadi wa millioni, kwahiyo mtu akisema 5 megapixels (5mp) ana maana pixels hizo ziko millioni 5.
Sasa ni nini maana ya pixels?
Hizi ni vidoti vidogo sana ambavyo vinakuwepo katika lens ya kamera ili kuweza kuonyesha details za picha itakayo pigwa nakuonekana inaeleweka na sio kufanya picha ionekane clear.
ANGALIA MFANO WA PICHA HII KWA MAKINI |
MFANO WA PILI |
JE NI MUHIMU SIMU KUWA NA MEGAPIXELS NYINGI?
Jibu ni hapana!!! labda kama unataka ku print picha zako ziwe zinakaa katika mabango barabarani, tumeona makampuni mengi ya simu yanakuja na *Selling Pitch* ya kuwa simu hii ina megapixels kadhaa so ni nzuri kwa ajili yako and blah blah.. kwa tulipo fikia saiz 13Mp zinatosha sana katika simu, tumeona kampuni kama SONY wametuwekea 21Mp, sio hao tu nokia walituwekea 42Mp, neno megapixels limekuwa ni kitu kinacho fanya makampuni yauze bidhaa zao kwa sababu wengi sana hawana uwelewa wa jambo hilo wakati inatakiwa ifahamike kuwa Sensor ya kamera ndio inafanya upate picha nzuri sana. kama tumeona mfano mzuri samsung walikua wanaiga tabia hii wakafika mpaka 16Mp lakini watu wengi wakashangaa simu yao mpya ya S7 ikaja na 12Mp sawa na walivyo fanya Nexus 6P lakini sensor zao ni nzuri na zinafanya picha iwe nzuri, na ni baada ya kujua sasa watu hawaangali namba wanaangalia uzuri ingawa Samsung hawajawahi kuangusha upande wa kamera.
NB; Megapixels zina patikana baada ya kuzidishwa kwa idadi zake kwa mfano
2MP= 1920x1080 etc
5MP=2592x1944 etc
3MP=2048x1536 etc
5MP=2560x1920 etc
Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall
Maoni yako Hapa chini