Friday, April 7, 2017

Jinsi ya Kufanya Livestreaming kwa kutumia VLC media player


Kama unatazama video au unasikiliza audio kupitia vlc basi unaweza fanya vifaa vya watu wengine kama simu au kompyuta zingine kuweza kuona mubashara kabisa kile ambacho unakitazama, ili uweze kutengeneza livestreaming station kupitia vlc fanya yafuatayo.

* Kompyuta yako na vifaa vinapaswa viunganishwe kwa kutumia WIFI hotspot moja ambayo inaweza kuwa ya simu au kompyuta.

* Fungua VLC media player yako, na kwenye menu bonyeza sehemu iliyoandikwa media na utaona sehemu iliyoandikwa "Stream", bonyeza na itatokea window kama hii



* kisha bonyeza hiyo sehemu iliyoandikwa "add" kuweka file ambalo unalotaka ku-stream.

 * Baada ya hapo bonyeza button sehemu iliyoandikwa stream ambapo itakuletea dialog ifuatayo,


*Kisha bonyeza button iliyoandikwa NEXT ambayo itakupeleka sehemu ambayo unayotakiwa kuchagua protocol.

*Utaona "Dropdown" menu ambayo ina protocols kazaa, unapaswa uchague protocol ya HTTP na kisha upande kulia utaona button ya add ibonyeze ili kuongeza hiyo protocol.

*uki-add itatokea namba ya poti(port) ambayo by default ni 8080,unaweza badili au ukaiacha kama ilivyo.


*kama uonavyo picha hapo juu, kisha hiyo sehemu ya transcoding options itoe(uncheck) hiyo alama ya tick, kisha bonyeza next, baada ya hapo usijaze chochote ila bonyeza button iliyoandikwa stream na kuanza kurusha video au audio mubashara kabisa.

NB: Unatakiwa ujue IP address ya kompyuta yako ili vifaa vingine viweze kustream file lako, ili kufahamu ip idress yako fungua cmd(command prompt)
kisha andika code ifuatayo

ipconfig /all

utaona IP yako mfano 192.168.43.1, kwa sababu ulichagua port number ya 8080 basi kifaa kingine chenye VLC watapaswa waingize IP mtindo huu, 192.168.43.1:8080

*basi hapo wataweza kuona video ama file lolote unalostream.

hakika VLC ni bonge la open source software.

Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top
Loading...