Sunday, December 3, 2017

Jinsi Hackers Wanavyoweza Ku-Hack Instagram


Instagram ni mtando maarufu sana duniani, na kupitia Instagram watu wanaweza kuonesha picha za mambo balimbali kwa watu wengine.


Instagram kama ilvyo mitandao mingine ya kijamii ili uweze kuitumia ni lazima uwe umejiunga nautatakiwa kuingiza jina na neno lako la siri ilikuweza kuitumia.

Na kwasababu hiyo basi account yako ya Instagram inaweza kuhackiwa/kuibiwa endapo tu password yako itatambuliwa na mtu asiyehusika.Sasa leo nitawaleza ni jinsi gani hackers wanaweza kuhack account yako ya Instagram.

TWENZETU!!!

1.APPLICATION AND PLUGINS- Ni kweli kuna application na plugins zinazoweza kutumika kuhack account yako ya instagram na mtandao wowote ule unaoutumia, ili hacker aweze kutumia browser plugin inampasa kuishika simu yako na na kisha kuziisntal hizo plugins kwenye browser yako, na plugins hizo zitasave password na majina yako unayotumia kuingilia instagram na kisa zitatumwa kwa hacker bila wewe kutambua lolote.

2.KEYLOGGERS- Hii ni moja ya software kubwa sana ambayo inatumiwa sana na hawa wezi wa mitandaoni(hackers). Na hacker atapaswa pia kuiinstal hii keyloger kwenye kifaa chako either ni simu au computer, na inawezekana akainstall bila kuishika simu au computer yako kabisa. Na keylogger ni vigumu sana kuitambua kama ipo kwenye kifaa chako kwani huwa haionekani kabisana haileti ishara yoyote lakini inakuwa inafana kazi kila wakati unapoitumia computer au simu yako na kuchukua kila unachokiandika na kukituma kwa hacker muhusika.

3.HARDWARE- Pia hackers baadhi wanatumia kifaa maalumu cha kugundua password kwa kujaribu maneno ambayo yanawezekana kuwa ni password ndani ya muda mchache sana ni kama ndani ya dakika moja kifaa hicho kinakuwa kimekwisha itambua password yako. Vifaa vya namna hii kweli vipo lakini havipatikani kirahisi sana na pia vina vinauzwa ghali sana.

4.HOOKING BROWSER and PHISHING METHOD- Huu ni ujanja mbao unawagharimu watumiaji wengi wa mitandao hiyo kama Instgram, kwa njia hii Hacker anaweza akafanya ukapata ujumbe wa ghafla ukiwa mtandaoni baada tu ya kutembelea tovuti fulani na huo ujumbe unaweza ukakutaka uingize jina na password yako ya instagram ujumbe unaweza kuwa "INSTAGRAM YAKO IMEPITWA NA WAKATI LOG IN ILI KUIDOWNLOAD MPYA", sasa baada ya kulog in tu hacker anapata jina pamoja password yako papo hapo napia kuna njia nyingi ambazo unaweza ukaibiwa account yako kwasababu tu ya uzembe na tamaa zako z mtandaoni, unaweza ukaambiwa ingiza jina na password yako ili upate followers zaidi ya 5000.

Lakini njia hii ya kutengeneza hizo jumbe inawezekana kwenye operating system ya KALI lINUX TUU 





Pata Makala Zetu Kwenye Simu Yako Kupitia Android Application ya Romanus Technology, Bonyeza Hapa Kuinstall

Maoni yako Hapa chini

Usipitwe Na Hii

Jinsi Ya Kupata "Likes" Nyingi Facebook

Watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakitamani kupata LIKES   nyingi kwenye status na picha zao wanazo post facebook lakini wameshindwa...

Back to Top